
Oktoba mwaka jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Google, Sundar Pichai alitangaza uwekezaji wa $1 billioni barani Afrika kwa ajili ya ukuajji wa huduma ya dijitali.
Kituo hicho kinaitaji watu wenye vipaji na ubunifu watakaoweza kusaidia kukuza maendeleo ya matumizi ya simu barani Afrika na kuboresha miundombinu ya huduma ya mtandao.
Watu watakaoajiriwa ni wahandisi, wabunifu na watafiti kwa lengo la kuzalisha bidhaa mpya na kukuza teknolojia kwa maendeleo ya Afrika na Dunia.