Jumatano , 8th Nov , 2023

Bilionea namba moja ulimwenguni Elon Musk, kupitia kampuni yake ya ''Neuralink'' wanatafuta watu ambao watakuwa tayari kujitolea ili kufanyiwa upasuaji wa kichwa kwa ajili ya kupandikizwa ''chip'' kwenye ubongo.

 

 Mfumo huu wa ''Neuralink'' unahusisha kuondoa kipande kidogo cha fuvu kwenye kichwa cha mgonjwa aliyekumbwa na maradhi ya kiharusi, na kupachika mfumo huu kupitia kifaa maalumu ili kusudi kimsaidie kurejesha hali ya uwezo wa kufikiri kama kompyuta.

Ijapokuwa kwa wagonjwa wa kiharusi kwa sasa wanatumia mfumo wa ''brain–computer interface (BCI)'' ambao unaunganishwa na fuvu la kichwa kwa msaada wa Akili mnemba (A.I) ambao unamuwezesha mgonjwa kuwasilisha mawazo yake kwa mfumo wa sauti.

Na mfumo huu kwa sasa unamuwezesha mgonjwa kuzungumza maneno 78 kwa muda wa dakika moja, lakini wanapanga kufanyia maboresho kumuwezesha mgonjwa kuzungumza maeneno 150 kwa lisaa.

Bado haijafahamika kama mfumo wa ''Neuralink'' utaweza kumsaidia mgonjwa zaidi ya mfumo huu wa Akili mnemba kupitia (BCI) pengine tusubiri matokeo ya majaribio yatasema nini kuhusu mfumo huu. 

Kwa mujibu wa wavuti wa Fox unaeleza watu wanaohitajika kwa ajili ya kujaribiwa kwenye mfumo huu wa ''Neuralink'' wanatakiwa 
* Awe chini ya umri wa miaka 40.
* Mwenye kusumbuliwa na kiharusi.
*Utayari wa mtu mwenyewe.

Picha: viniloblog.com