Facebook na ujio mpya wa huduma ya mahusiano

Ijumaa , 6th Sep , 2019

Facebook wameanzisha huduma mpya, maalum kwaajili ya kuanzisha mahusiano ya ukaribu zaidi baina ya watumiaji wa mtandao huo kama mapenzi na mengineyo.

Huduma hiyo tayari imeanza kupatikana katika nchi kadhaa kama Marekani, Colombia, Thailand na inatazamiwa kuanza kusambaa katika nchi nyingine hivi karibuni.

Huduma hiyo kwa sasa inapatikana katika App kuu ya Facebook hivyo mtumiaji kama unataka kujiunga, itakupasa kuunda wasifu (profile) yako nyingine na utaanza kuona marafiki kadhaa ambao wataanza kuonekana kutokana na mfanano wa taarifa mlizoweka.

Kupitia Instagram pia kipengele hicho kitaongezwa na kupewa jina la "Secret Crush", ambayo itakupa uwezo wa kuwaorodhesha marafiki zako wote kadhaa kwa siri ambao unawapenda na wao wakikubali ombi au kukuorodhesha basi mnaweza kuanzisha uhusiano wenu mnaokusudia.

Mtandao wa Facebook kwa siku za hivi karibuni umekuwa ukituhumiwa kuvujisha taarifa za watumiaji wake hivyo uanzishwaji wa huduma hiyo wachambuzi mbalimbali wa masuala ya mitandao wanaona huduma hiyo usalama kwa watumiaji unaweza ukawa sio rafiki sana.

Facebook kwa upande wao wamesema hawana mpango wowote wa kutumia huduma hiyo kwaajili ya mambo ya kibiashara au kutumia taarifa za watumiaji wake vibaya kama wengi wanavyohisi.