Fahamu Gauni la Bilioni 11

Jumatano , 12th Mei , 2021

Gauni la ‘Happy Birthday Mr. President’ la Marilyn Monroe ndilo vazi linaloshikilia rekodi ya kuuzwa ghari zaidi katika historia ambapo mwaka 2016 makumbusho ya “Ripley's Believe It or Not”  walilinunua kwa $ 4.8 milioni sawa na TSH 11 Bilioni.

Picha ya Gauni ‘Happy Birthday Mr. President’ likiwa makumbusho ya Ripley's Believe It or Not

Mei 19,1962 siku 10 kabla ya sherehe ya kuzaliwa ya miaka 45 (birthday) ya aliyekuwa Rais wa 35 wa Marekani John F. Kennedy,  mwanamuziki na mitindo huyo alivaa vazi hilo alilolipia $1.4 sawa na milioni 3.3, kwenye shughuli ya ukusanyaji wa fedha kwa Rais na Kamati ya Kitaifa ya Kidemokrasia pale “Madison Square Garden”,  sasa wakati akiimba wimbo wa kumtakia kheri Rais ndipo likapewa jina la ‘Happy Birthday Mr. President’.

Ikumbukwe kwa mara ya kwanza Gauni hili lilipigwa mnada mwaka 1999 baada ya kushinda zabuni ya $1.3 milioni sawa na TSH 2.9 Bilioni