Jumatano , 13th Mei , 2020

Terry Gobanga alizaliwa nchini Kenya, amesimulia kisa chake cha kubakwa na wananume watatu na kumjeruhi na kisu tumboni masaa machache kabla ya ndoa yake, kitendo ambacho kilibadilisha maisha yake, lakini mwanaume alimngoja na alipopona miezi 7 baadaye Julai 2005 walifunga ndoa.

Terry Gobanga

Terry anaeleza kuwa kisa cha kubakwa kwake, kilitokea majira ya asubuhi baada ya kumsindikiza rafiki yake kituo cha basi, aliyekuwa anaenda kumpelekea mchumba wake Terry tai na vitu vingine ambavyo alitakiwa kuvivaa siku hiyo.

Hakuna aliyeamini baada ya kusikia taarifa hizo, kwani watu walikuwa wameshafika kanisani lakini walishangaa kutomuona bibi harusi, wakati wabakaji walipomtupa, tukio hilo lilishuhudiwa na mtoto mdogo aliyepiga yowe kuomba msaada na hata Polisi walipokuja walidhani amekwishafariki lakini baadaye walimkimbiza hospitali.

Terry anaeleza kuwa baada ya siku 29 za ndoa yake, mume wake huyo alifariki Dunia baadaye baada ya kuvuta hewa ya Carbon-monoxide, kutokana na kulala na jiko la mkaa ndani kwakuwa maeneo waliyokuwa wakiishi yalikuwa na baridi sana.

Kitendo cha Terry kufiwa na mume wake kilimuumiza sana hali iliyopelekea yeye kukata tamaa ya kueolewa tena, ambapo baadaye alikutana na mwanaume mwingine aliyejulikana kwa jina ya Tonny Gobanga aliyemuomba amuoe na awe mke wake, ilikuwa ni miaka mitatu tangu harusi yake ya kwanza, kwahiyo Terry alikuwa na uoga pamoja na hofu kuu kuhusu ndoa nyingine , hususani kwa mume mwingine.

"Kwahiyo nilisema ndiyo na kukubali Tonny anioe ila Tonny alipowaeleza wazazi wake kuhusu azma hiyo kwa kujua kilichonikuta walimkataza kunioa, licha ya hayo harusi ilifanywa japo baba mkwe hakufika katika harusi yetu, watu 800 walifika lakini naamini wengi walifika kushuhudia harusi yangu kutokana na matukio ya maisha yangu ya hapo nyuma " amesema Terry.

''Mwaka mmoja tangu ndoa , nilianza kuhisi vibaya , lakini nilipokwenda hospitalini Daktari aliniambia kuwa nilikuwa na ujauzito , kwa kweli nilishtuka nisijue cha kufanya'' ameeleza Terry.

Na baada ya muda alijifungua mtoto wa kike na baada ya miaka mingine minne, alibarikiwa kupata mtoto wa pili na Terry kwa sasa anaishi na mume wake nchini Marekani katika jimbo la Texas.

Chanzo:BBC