Ijumaa , 20th Mei , 2022

Kampuni ya Mercedes-Benz siku ya jana iliweka rekodi ya kuuza gari la gharama zaidi Duniani, kwa kuuza gari lake aina ya Mercedes-Benz 300 SLR ‘Uhlenhaut Coupe’ ya mwaka 1955 kwa kiasi cha dola milioni 142 sawa na Tsh bilioni 330.

Mercedes-Benz 300 SLR ‘Uhlenhaut Coupe’

Kabla ya hapo gari aina ya Ferrari 250 GTO ya mwaka 1963 ndiyo lilikuwa gari la gharama zaidi, mwaka 2018 liliuzwa kwa kiasi cha dola milioni 70 sawa na Tsh bilioni 163.

Pesa zilizopatikana katika mauzo ya gari hii zitatumika kuanzisha mfuko wa Mercedes Benz kwa ajili kusaidia ya wanafunzi katika masomo ulimwenguni.