Harusi yafanyika bila chakula Kenya

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Imezoeleka kwenye kila sherehe nyingi lazima kuwe na vinogesho kama chakula, vinywaji, muziki na 'surprise' zingine lakini hiyo imekuwa tofauti kwa wanandoa Amos Mburu na Mary Wairimu ambao wamefunga ndoa na kualika watu bila ya kutoa chochote kwa wahudhuriaji.

Baadhi ya mpangilio wa kupewa chakula kwenye harusi au sherehe zingine

Wanandoa hao kutoka Kaunti ya Nakuru nchini Kenya waliwaacha midomo wazi baadhi ya wageni 30 waliowaalika kwenye harusi yao bila ya kuwaburudisha.

Mmoja wa wageni hao walioalikwa ambaye ni mwanamke alisikika akisema "Tumezoea kupata wali na nyama lakini leo tumekaa hapa na njaa, tutarudi nyumbani na njaa kila mtu atakula kwao"

Aidha kwa upande wa Bwana harusi Amos Mburu amesema alitamani kuona harusi yake ikihudhuriwa na watu wengine ila kulingana na sheria zilizowekwa ili kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona imefanya kualika idadi ya watu wachache.