Jumatatu , 6th Nov , 2023

Ni muda sasa wa kusema changamoto ya muda mrefu imepata mtatuzi, lakini hofu yetu ni kwamba tutaweza kutengeneza watu waliobora kwenye somo la hisabati tena?

 

Linabaki kuwa swali lisilo na majibu,

Mtandao namba moja kwa watumiaji Duniani, Mtandao wa ''Google'' umefanya baadhi ya maboresho kwenye utafutaji wa kawaida na ule wakutumia ''Lens'' ndani ya mtandao huo,

Ila kubwa ni kwenye maboresho yaliyohusiana na ''Google Lens''

Hii ''Google Lens'' ni kile kialama cha kamera unachokiona unapoingia kwenye ''Search ya Google'' kutafuta kitu, na kile kinakusaida kwenye kupata kufahamu vitu vikiwa kwenye maumbo na muonekano zaidi.

Awali ilikuwa haina uwezo wa kukokotoa maumbo, lakini maboresho mapya yaliyofanyika ndani ya ''Google Lens'' yanamruhusu mtumiaji wake kupata majibu ya maswali yaliyo kwenye maumbo ndani ya hisabati.

Siyo tu kwenye somo la Hisabati hata pia kwenye somo la fizikia kwenye baadhi ya michoro,

Unachotakiwa kufanya ni kuchora ''equation'' husika, alafu ''Google Lens'' itafanya sehemu yake ya kukupa swali, kazi na jibu hapo umekumbuka mbali kidogo.

Si lazima kuchora hata ile ambayo iko kwenye karatasi au vitabu tayari, utachofanya ni kumulika kama unapiga picha na yenyewe itafanya kazi yake.

Picha: iStock