Jumanne , 15th Nov , 2022

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) idadi ya watu Duniani imefikia bilioni 8, ikiwa watu bilioni 1 wameongezeka ndani ya miaka 11.

Ikiwa ni miaka 11 imepita tangu Dunia ilipofikisha watu bilioni 7.

Watu milioni 700 wameongezeka katika bara la Asia tangu mwaka 2011, ikiwa idadi kubwa ya watu wameongezeka kutokea nchini India ambapo watu milioni 180 wameongezeka na nchi hiyo inatarajia kuipita China kwa idadi ya watu ifikapo 2023.

Inatabiriwa kuwa Dunia itafikisha idadi ya watu bilioni 9 ifikapo 2037 na watu bilioni 10.4 ifikapo 2080.