Alhamisi , 25th Jan , 2024

Mkurugenzi mtendaji wa Instagram Adam Mosseri, ametangaza maboresho mapya kutoka kwenye application ya Instagram ambayo yanamruhusu mtumiaji wa appplication hiyo kuzuia kuonekana iwapo ujumbe uliyotumwa mpokeaji ameusoma au la,

 

Hii siyo ngeni kwa watumiaji wa ''WhatsApp'' kwani inafahamika kama ''read receipts'' kuiyelezea kwa ufupi ni kwamba ujumbe unamfikia mpokeaji na anausoma, lakini mtumaji huwezi kufahamu kama ujumbe huo umemfikia muhusika.

Kwa sasa Instagram nayo inafanya majaribio ya kuja na huduma hii, kwa watumiaji wake na kwa sasa iko kwenye hatua ya majaribio kwa watumiaji wachache wa ''beta''

Na itakapo kamilika ili kuwezesha huduma hii kwenye account yako ya instagram, utaingia kwenye Privacy & Safety kwenye upande wa settings na kuchagua chaguo lililoandikwa off the Read Receipts.

Kwa WhatsApp iwapo mtumiaji atatumia huduma hii si yeye pekee ambaye hatofahamika kama amesoma ujumbe wa mtumaji lakini pia yeye hatoweza kutambua kama ujumbe aliotuma umepokelewa au la, kingine ni hatowezeshwa kufahamu kama status aliyoweka imetazamwa na watu wangapi.

Bado haijafahamika kwa instagram itakuwaje, tuendelee kusubiri.

Kwa upande wako mwana-tech unahisi itakuwesha kukuza usalama wako utakapo kuwa mtandaoni? tuandikie mtazamo wako kwenye hili.

Picha: deasilex.com