Jumanne , 14th Nov , 2023

Kwa asilimia kubwa ukiona sheria imeundwa basi tambua yupo ambaye alijaribu kuvuka mipaka, hii haina tofauti sana na uvumbuzi wa kisayansi. 

 

Kila ambapo kulitokea changamoto basi ilitafutwa namna rahisi ya kukabiliana na changamoto hiyo, hadithi ya namna mkanda wa kiti cha gari ulivyopatikana inaweza kukushangaza kidogo.

Uliwahi kusikia hata aliyegundua gari alikufa kwa ajali, huu ulikuwa ni mstari wa Mwana Fa (Mheshimiwa Naibu Waziri); lakini alikuwa hana maana hiyo,  ila ni namna ya kutengeneza ujumbe kwa njia ya sanaa.

Lakini mstari huo unaweza ukachukua sehemu ndogo ya uhalisia, kwani mwaka 1958 baada ya kutokea kifo cha mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Volvo; Gunnar Engelau kufariki kwa ajali ya gari.

Ndipo mhandisi kutokea kampuni hiyo anayefahamika kama Nils Bohlin alipewa jukumu la kubuni na kuja na njia mpya na salama zaidi mtu atakapokuwa anatumia gari hizo.

Ndipo wazo la mkanda wa kiti kwenye gari likaanzia hapo; Ijapokuwa imepitia maboresho mengi mpaka kupata mkanda unaotumika kwenye magari ya kisasa.

Kila ifikapo tarehe 14/11 kila mwaka huwa ni maadhimisho ya kufunga mkanda wa kiti kwenye gari, siku hii imewekwa maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha watu umuhimu wa kufunga mkanda wa kiti wawapo kwenye gari.

Kwani kufanya hivyo kunasaidia kupunguza changamoto za ajali ambazo pengine zinge epukika endapo mtu angefunga mkanda kwenye chombo cha usafiri.

Picha: andywins.com