Alhamisi , 5th Mei , 2022

Mfahamu Kijana wa miaka 13 kutokea Uingereza, Omari McQueen anaetengeneza mkwanja kupitia mitandao ya kijamii kwa kutengeneza video za mapishi, pia kipindi chake cha 'What’s Cooking Omari?' kinaruka kupitia channel ya watoto ya BBC kwa msimu wa pili.

Omari anamiliki kampuni yake mwenyewe inayoitwa 'DIPALICIOUS'

Omary alifundishwa kupika na baba yake tangu akiwa na umri wa miaka 7, alipofika miaka 10 aliomba wazazi wake ajiunge na mtandao wa LinkedIn, baadae akajiunga YouTube na kuanza kutengeneza maudhui.