Kilichokuwepo nyuma ya Monalisa na Amina Chifupa

Ijumaa , 5th Jun , 2020

Muigizaji wa BongoMovie Monalisa, amefunguka kuhusu kushea mwanaume na marehemu Amina Chifupa, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM, na mwanaume mwenye alikuwa ni marehemu Mohamed Mpakanjia.

Msanii wa filamu Yvonne Cherrie "Monalisa"

 

Akipiga stori kwenye show ya SalamaNa ya East Africa TV inayoruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku amesema  "Mimi na Amina Chifupa tulikuwa marafiki  wazuri, yeye alikuwa anasoma Kisutu mimi Zanaki ila tulikuwa tunakutana sana, kilichotukutanisha zaidi ni Mohamed Mpakanjia,  na mimi binafsi nilianza mahusiano na Mpakanjia kabla ya yeye".

"Baadaye nikaja kusikia ninayetembea naye ni mume wa mtu ila hakuwahi kuniambia kama ana mke, nikaanza kumpunguza na kumpotezea taratibu japo ilikuwa ngumu, halafu nikasikia anatoka na Amina Chifupa na kuna siku Amina alinitafuta akaniambia kwamba hakujua kwamba mimi nilikuwa naye kabla yake" ameongeza.

Aidha Monalisa ameendelea kusema  "Siku anayofariki Amina Chifupa, mimi nilikuwa nimetoka kujifungua mtoto wangu wa pili kwahiyo sikuweza kwenda msibani, iliniuma sana kwa sababu alikuwa ni mchapakazi".

Marehemu Amina Chifupa alifariki Juni 26, 2007, ila aliolewa na mfanyabiashara Mohamed Mpakanjia ambaye naye alifariki mwezi Septemba 2009.