Jumatatu , 6th Nov , 2023

 Unasifika kwa kuwa na watumiaji zaidi ya Bilioni 2 ulimwenguni kote, huku ukiwa na watu zaidi ya milioni 39 waliopakua ''Application'' hii, ukishika nafasi ya nne baada ya Facebook, Instagram na TikTok.

 

WhatsApp kwa sasa wanafanya majaribio ya kuwaruhusu watumiaji wake kuingia kwenye ''account'' zao za WhatsApp kwa kutumia E-mail ikiwa kama mbadala wa namba ya simu.

Kwa lugha nyepesi hautakuwa na haja ya kuweka laini yako ya simu kwenye kifaa chako ili kupata namba sita ''OTP'' ambazo hutumika kama udhibitisho kwako unapoingia kwenye ''account'' yako kwenye mtandao wa WhatsApp.

Hii haina maana ya kutambulishwa kwa mfumo wa E-mail kutaondoa mfumo wa ''OTP'' bali itamuongezea machaguo zaidi mtumiaji wa mtandao wa WhatsApp. 

Kwa Lugha nyepesi hiki  ambacho kimeandikwa hapa ni kama unapopika, mwanzoni ilikuwa lazima upike Pilau ndiyo watu wafurahie chakula lakini inakuja namna nyepesi ya wali mweupe ambao haitaji viungo kukamilisha pishi hili, bali ni mchele uleule ambao hapa umekuja kwenye namna ya tofauti. 

Picha: @pinterest.com