Ijumaa , 13th Mei , 2022

Fundi umeme, Tony Finn aliyefanya kazi katika kampuni mmoja huko Uingereza kwa miaka 24 kabla ya kufukuzwa kazi mwezi Mei mwaka jana, aliifikisha mahakamani kampuni hiyo kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Tony anadai alifanyiwa tukio hilo mwaka 2019.

Baada ya kufukuzwa kazi alimfungulia kesi bosi wake wa zamani, kwa madai aliwahi kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia mwaka 2019 akiwa kazini kwa kumdhihaki muonekano wake hana nywele kichwani.

Aliipeleka kampuni hiyo mahakamani akidai amekuwa mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia baada ya kugombana na msimamizi wa kiwanda hicho, Jamie King.

Tony ameshinda kesi yake baada ya jaji wa mahakama Jonathan Brain, kutoa uamuzi kuwa, kumwita mtu ana upara ni unyanyasaji katika eneo la kazi kwa mujibu wa sheria za ajira nchini Uingereza.