Jumapili , 19th Nov , 2023

Kila ifikapo tarehe 19/11 kila mwaka huadhimishwa siku ya Wanaume Duniani, kuadhimishwa kwa siku hii ni kwa lengo la kutambua yale yote anayopitia mwanaume kwenye jamii yake, 

 

Mjadala unakuwa mzito kidogo ikifika maadhimisho ya siku kama hii kwani hali ni tofauti kabisa na yale maadhimisho ya tarehe 8/3 (siku ya wanawake ) 

Baadhi ya wadau wanaenda mbali kwa kuhisi labda, pengine siku hii kuingiliana na maadhimisho ya siku ya choo duniani ndiyo sababu ya kuto kuadhimishwa kwa ukubwa zaidi?

wewe mtazamo wako kwenye hili ni upi, Unahisi ni kwa nini siku ya wanaume Duniani haiadhimishwi kwa ukubwa?