Jumatano , 25th Oct , 2023

Kwenye upande wa afya mwezi wa 10 kila mwaka ni mwezi ambao ulitengwa makhususi kwa lengo la kuzungumza na kujadili kuhusiana na saratani ya mapafu (Lung cancer).

 

Na kila Jumatano ya nne ya mwezi wa 10 ndiyo maadhimisho rasmi ya kuhusiana na saratani ya mapafu, Lengo likiwa ni kuwafahamisha na kuwajulisha watu kuhusiana na ugonjwa hatari wa kansa ya mapafu.

Kwa mujibu wa tafiti za mwaka 2020 za shirika la afya ulimwenguni (WHO) zinasema saratani ya mapafu, Ni namba mbili kwa kuwapata watu ulimwenguni; huku namba moja ikiwa kansa ya matiti yaani (Breast cancer)

Baadhi ya vitu ambavyo unatakiwa kufahamu kuhusiana na kansa ya mapafu, kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni.

- Kansa ya mapafu ndiyo kansa inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo.

- Uvutaji wa sigara, siga na shisha hupelekea kiwango kikubwa cha maambukizi ya kansa ya mapafu (kwa karibu ya asilimia 85).

- Saratani ya mapafu mara nyingi hugunduliwa katika hatua za mwisho wakati mgonjwa yuko katika hali mbaya.
- Kwa mujibu wa tafiti kutoka wavuti wa ''CDC'' unasema 10% hadi 20% (ambao ni sawa na watu 20,000 hadi 40,000) ya wagonjwa ambao hukumbwa na kansa ya mapafu ni wale ambao hawakuwahi kabisa kuvuta na wale ambao walivuta lakini sigara chache zaidi.