Ijumaa , 8th Dec , 2023

Tuzo za mwezi ''November'' kwenye ligi kuu ya uingereza, zimetoka na Klabu ya Manchester United kuwa kinara kwenye tuzo hizo,

kwa kutoa mchezaji bora wa mwezi, Kocha bora wa mwezi na pia goli bora la mwezi.

Kocha wa Timu hiyo, Erik ten Hag ametambuliwa kama kocha bora wa mwezi November,

Goli la Alejandro Garnacho kwenye mchezo wa Manchester United dhidi ya Everton (bicycle kick) limetambuliwa kama goli bora la mwezi November,

Harry Maguire ametambuliwa kama mchezaji bora wa mwezi 11,

Ni sahihi kusema ''Man U'' hii ndiyo gari limewaka?