Jumanne , 14th Nov , 2023

Vuta picha unaamka asubuhi, alafu unafahamishwa kila kinachoendelea duniani kwa muda huo; kwa njia ya sauti, au unahitaji kujua ni kitu gani mtu kazungumza ikiwa lugha aliyozungumza ni tofauti na ya kwako, basi unasikia kitu kile kile kwenye lugha yako kwa muda huo huo.

 

Humane’s Ai Pin ni nini?
Ni kifaa ambacho huvaliwa kwenye nguo na kimeundwa kuja kuwa mbadala wa simu janja. Kifaa hiki hufanya kazi kama kompyuta na kina ''sensor'' ndani yake ambayo inawezesha kufanya kazi kwenye uhalisia wa mwanadamu.

Kifaa hiki kinamuwezesha mtumiaji wake kupiga picha, kutuma ujumbe (text) na kuonyesha baadhi ya vitu kama vile kubadili muziki unaosikiliza kupitia kiganja cha mkono.

Kubwa zaidi kuhusu kifaa hiki kimewezeshwa akili mnemba maarufu zaidi inayofahamika kama ChatGPT ambayo kwa sasa inafikia zaidi ya watumiaji Milioni 100 kwa kila wiki.

Inafanyaje kazi?
Ukisha nunua na kukamilisha kufanya ''setting'' kwa maana ya kuunganisha na simu yako ya mkononi, unaweza kuuliza swali na kukamilisha mengi unayohitaji kutoka kwenye kifaa hicho kwa kutumia kiganja cha mkono kwani hutoa mwanga kama ilivyo ''projector'' hivyo inakuwa kama sehemu ya wewe kufanya machaguo na kuendesha kutokana na hitaji husika la muda huo.

Gharama yake ipoje?
Ikiwa kama ndoto yako kumiliki kifaa hiki basi kitapo tangazwa rasmi kwamba kinapatikana sokoni kwa sasa basi fahamu gharama yake, Ni Shilingi Milioni 1.7 Tsh, lakini ni kama huduma ya kisimbuzi hii Ai Pin utahitajika kulipia kila mwezi kiasi kisichopungua shilingi elfu 60,000 kwa ajili ya kulipia storage na akili mnemba inayotumika kwenye kifaa hicho.

Faida zake ni zipi?
Inajifunza kutokana na mzunguko wako wa kila siku kwenye maisha, ni rahisi kuitumia kwani ni sauti yako kwa asilimia kubwa, Inakusaidia kwenye maswala ya lugha kwenye kuwasiliana na watu, Pia unaunganisha na vifaa vyako kama vile TV, fridge, gari nk. rahisi zaidi unapachika tu kwenye nguo yako.

Hasara zake ni zipi?
Gharama yake ni kubwa mnoo hivyo inawia ugumu watu wengi kuimudu, haina ubunifu wa kutosha kwani maamuzi yake ni kutokana na yale ambayo yalikwisha wahi kutokea nyuma. 

Mmiliki ni nani?
Umiliki wa ''Human A.I pin'' unajumuisha wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Apple Inc mmoja ni Imran Chaudhri ambaye alifanya kazi kwenye kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 21, mwingine ni Bethany Bongiorno ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 8, Baada ya kutoka kwenye kampuni hiyo ndiyo wakaanzisha kampuni yao.

Picha: Time.com