Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mkuu wa mkoa ataka maiti zifufuliwe

Jumatatu , 29th Oct , 2018

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka waganga wa kienyeji maarufu kama lambalamba mkoani humo kwenda kuwafufua watu waliofariki dunia, ndipo atakapowaruhusu kuendelea na kazi yao ya kutoa uchawi.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Mh. Chalamila amesema kwamba ameamua kutoa agizo hilo baada ya wananchi kumuomba awaruhusu waganga hao kufanya kazi yao ya kutoa uchawi, jambo ambalo serikali haiamini.

“Walileta maombi maalum kuwa serikali iwaruhusu huku wakitoa ushuhuda watu hao wakitoa uchawi, kutoa baadhi ya vitu na kuponya watu, ndipo mimi niliposimama nikasema haitawezekana,  nikawaambia kama mnawashukuru wanaowaponya, nitawaruhusu kwa masharti, tukutane nao mochwari katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, wanifufulie maiti zilizopo pale, kwa ushuhuda huo nitawaruhusu kweli ni waponyaji katika ulimwengu wa roho”, amesema Chalamila.

Mh. Chalamila aliendelea kwa kusema kwamba iwapo watu hao wataweza kufanya kazi zao kisayansi yenye kuleta manufaa, hatosita kuwaruhusu kuendelea kufanya shuhuli zao zenye imani ya kishirikina.

"Mimi nataka kwa sayansi, wakinisaidia hilo nitawaruhusu, kwa mfano mtu anataka kuwahi Dar es salaam wakanionyesha nitakubali, au walete mvua wakati wa kiangazi tumwagilie mazao yetu, wanaopotea waseme wako wapi, mimi nataka hilo”, amesema Mh. Chalamila.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali