Ijumaa , 24th Mei , 2019

Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizozichukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019, ambapo kwa kipindi  cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki.

Picha yenye Nembo ya mtandao wa Facebook.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg,, amewakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ifungwe, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

"Sidhani kama suluhisho ni kuifunga kampuni kwasababu tunashughulikia hili tayari na ni changamoto za kibiashara", amesema Zuckberg.

Karibia watumiaji 150,000 walifunguliwa akaunti zao baada ya kubainika kuwa hawakukiuka sheria kipindi hicho. 
Facebook imesema ripoti hiyo imeangazia masuala hayo ili kuendesha huduma zake kwa njia ya uwazi na uwajibikaji ili kuufanya mtandao huo kuwa salama kwa wateja wake.