Jumanne , 1st Oct , 2019

Kenna Ngoma linaweza likawa si jina maarufu kwa Watanzani wengi, lakini kwenye soka la Uingereza na klabu ya Manchester City ni jina kubwa ambalo lilikatisha ndoto za kucheza soka na sasa ni mfanyabiashara mkubwa.

Kenna Ngoma wa pili kutoka kulia waliosimama, akiwa kwenye Academy ya Man City alipokuwa na miaka 14.

Kenna Ngoma ni Mtanzania ambaye anaishi jijini Manchester akifanya biashara ya Ice Cream ambazo zimemuweka kwenye ramani ya dunia, baada ya kutajwa kwenye orodha ya watu 16 wanaowania kuibuka kinara kwenye shindano la 'The Apprentice 2019'.

Kenna Ngoma (wa 4 waliosimama juu) akiwa na washiriki wenzake.

Kenna Ngoma ana umri wa miaka 24, ni mmiliki wa kampuni ya  Ice Cream zenye kilevi na aliianzisha mwaka 2018 ambapo mpaka sasa inafanya vizuri.

Kabla ya kuwaza kuwa na kampuni hiyo, akiwa na umri wa miaka 12, Kenna Ngoma alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu ambapo alipita kwenye vituo kadhaa vya kukaza vipaji vya soka kama Barnsley Academy ambapo alicheza na mlinzi wa kati wa Man City John Stones.

Kenna Ngoma (wa 4 kutoka kushoto waliochuchumaa) akiwa Barnsley Academy)

Kenna ambaye wazazi wake walihamia Uingereza kutoka Tanzania alipokuwa na miaka mitano, alikuwa akicheza mpira mpaka mwaka 2013, akiwa na umri wa miaka 17,  kwenye Academy ya Man City. Lakini aliumia na maumivu hayo yalikatisha ndoto yake ya kucheza soka na kuamua kufanya shughuli zingine.

Katika shindano hilo ambalo lipo kwenye msimu wake wa 15, litaanza kuruka rasmi kesho Oktoba 2, 2019 ambapo washiriki 16 akiwemo Kenna watakuwa wanashindana kuwania nafasi ya kushinda kufanya biashara ya mfanyabiashara mkubwa Lord Alan Sugar.

Mbele ni Lord Alan Sugar ambaye atashirikiana kibiashara ya mshindi.

Shindano hilo ambalo litakwenda kwa wiki 12, mshindi atakabidhiwa kitita cha £250,000 zaidi ya shilingi Milioni 705,699,714. Pia atamiliki kampuni mpya kwa kugawana asilimia 50 na mfanya biashara Lord Alan Sugar.

Kenna Ngoma