Jumanne , 23rd Jan , 2024

Kulingana na utafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford, kuwa na marafiki na kupata moja moto moja baridi siyo tu hufurahisha wanaume, bali pia ni muhimu kwa afya zao.

 

Mwanasaikolojia Robin Dunbar, kwa kushirikiana na kikundi cha utafiti wa maswala ya ''neuroscience'' kutoka chuo kikuu cha Oxford, wamebaini kuwa mwanaume anahitajika kupata mtoko angalau mara mbili katika wiki, ili kukuza ustawi wa urafiki na kwa afya yake binafsi.

Dunbar anasema urafiki wa mwanaume unaweza kukua kwa kushiriki kwenye mambo mbalimbali na wanaume wengine, ikiwa ni pamoja na maswala ya kimichezo, kupata moja moto moja baridi na aina nyingine zinazopelekea makutano ya wanaume.

Utafiti wao ulibaini kuwa wanaume ambao walistawisha uhusiano wao kwa maana ya kukutana angalau mara mbili kwa wiki na marafiki zao, walikuwa na asilimia ndogo sana ya kupatwa na msongo wa mawazo ambao mara nyingi, utokea kutokana na ukosefu wa kazi kwa mwanaume, kukosa fedha (hali mbaya ya kiuchumi) na mengineyo

Kwa nyiongeza walibaini kuwa wale ambao walifanikiwa kukutana na marafiki angalau mara mbili kwa wiki walifanikiwa kurejea kwenye hali ya kawaida kwa uharaka zaidi pale walipokumbwa na msongo na upweke ukilinganisha na wale ambao hawajichanganyi na marafiki.

Picha: food24.com