Jumamosi , 6th Mar , 2021

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idris Sultan, amesema kuwa mwanamke ni kiumbe ambaye anaipa Dunia kila kitu anachokipenda na kwamba Mungu asingekuwepo basi yeye angeabudiwa.

Mchekeshaji Idris Sultan

Katika kuelekea siku ya wanawake Duniani inayofanyika kila mwaka ifikapo Machi 8 kila mwaka, ameyaandika hayo hii leo Machi 6, 2021, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Mwanamke anaipa Dunia kila anachokipenda kuanzia busara, malezi na mpaka mtoto wa kutoka tumboni mwake, kusingekuwa na Mungu basi yeye ndiye angeabudiwa," ameandika Idris.