Alhamisi , 6th Feb , 2020

Mchungaji wa kanisa la GRC, Antony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, amemtetea Mtume Boniface Mwamposa , kwamba tukio alilolisababisha la watu zaidi ya 20 kupoteza maisha sio la imani potofu kama kafara au freemason.

Pichani kushoto ni Mchungaji Mzee wa Upako, kulia ni Mchungaji Mwamposa

Mzee wa Upako amesema Mwamposa hakuwakimbia Polisi, bali alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Oysterbay.

"Mwamposa amezushiwa, kawaida anapomaliza mikutano yake siku ya Jumamosi awapo mikoani huwa anawahi kurudi Dar es Salaam kwa ajili ya ibada ya Jumapili, na aliposikia yaliyotokea akaenda kujisalimisha kituo cha polisi Oysterbay, yeye sio freemason wala kutaka kutoa kafara, ila kama kuna kesi ya jinai ashtakiwe" amesema Mzee wa Upako.

Aidha Mzee wa Upako amesema yeye alianza kazi hii ya kuhubiri mnamo mwaka 1972, japo watu walikuwa wanampinga kwa kumwambia kwamba yeye ni mdogo, sasa hivi ana miaka 36 kwenye kazi hiyo.