Jumatatu , 8th Jan , 2024

Ipo nadharia moja ambayo inafahamika kama “The Red Car Theory” 

Purukushani za watoto kurudi shule leo hii. huwenda ukawa umetumia muda mwingi barabarani, lakini vipi nikikuuliza umepishana na magari mangapi, yenye rangi nyekundu leo?

 

Inaweza kuwa ngumu kukumbuka kwa sababu hukuwa umetilia maanani au kuweka umakini wa kutaka kufahamu ni magari mangapi yenye rangi nyekundu umepishana nayo siku ya leo.

Sasa hii ndiyo inahusianishwa moja kwa moja na nadharia hii inayofahamika kama “The Red Car Theory” nadharia ambayo inahusu uhalisia wa maisha ya mwanadamu, kwenye upande wa kuzitazamia fursa.

Kuieleza kwa ufupi “The Red Car Theory” inaeleza kuwa fursa ni nyingi lakini mara nyingi tunapishana nazo kwa sababu hatuzitafuti kwa ukamkilifu au kuzitilia maanani, tunabaiki kupishana nazo kila uchwao.

Na hii ndiyo maana ya swali hapo juu, lililouliza kuhusu ni magari mangapi yenye rangi nyekundu uliyopishana nayo kwa siku ya leo.

Cc: fatrank.com