Jumanne , 30th Jan , 2024

Kampuni ya Neuralink inayomilikiwa na tajiri nambari mbili duniani, Elon Musk imefanikiwa kupandikiza kifaa cha kiteknolojia kwenye ubongo wa mwanadamu.

 

 

Ingawa hajatoa maelezo kamili ya mgonjwa wala kifaa hicho, ila inatajwa kuwa ni hatua muhimu kwa kifaa kinachoitwa ‘Telepathy’, chenye uwezo wa kumruhusu binadamu kutumia simu au kompyuta kwa njia ya kufikiria.

Akieleza kuhusu upandikizaji huo kupitia mtandao wa X Elon ameeleza kuwa Binadamu wa kwanza amepokea kipandikizi kutoka Neuralink mapema siku ya juz kwa mujibu wa kampuni hiyo mtu huyo na anaendelea vizuri

 

Kampuni hiyo ilipata idhini kutoka mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani (FDA), kufanya jaribio lake la kwanza mwaka jana ambapo ilitangaza kutafuta watu wa kujitolea kupandikizwa.

 

Kupitia Neurotechnology iliyoanzishwa na bilionea huyo mwaka 2016, kampuni hiyo inalenga kujenga njia za mawasiliano ya moja kwa moja kati ya ubongo wa mwandamu na kompyuta.

 

Picha: viniloblog.com