Jumatano , 25th Oct , 2023

Mmiliki wa mtandao wa META, ndugu Mark  zuckerberg kwenye mahojiano yake na mtandao wa ''verge'' amefunguka kwa kusema kabla ya kununuliwa na Elon Musk

moja kati ya vitu ambavyo aliwahi kuzungumza na mmlikiwa wa mtandao ''Twitter '' zamani ''X'' kwa sasa Bwana Jack Dorsey ni kuhusiana na yeye kununua mtandao huo.

''Niliwahi kuwa na mazungumzo na Jack kuhusu hilo kabla ya kutoka kwenye nafasi yake ya awali, lakini nadhani kila mjasiliamali yuko na malengo ya tofauti, kwa sasa Elon ni kama wakala wa mabadiliko tangu amenunua amebadilisha baadhi ya vitu kwenye mtandao huo, binafsi naweza kuwa na matumaini kidogo au nadhani kuna nafasi ndogo sasa kuliko ilivyokuwa hapo awali''

Mark amejaribu kuweka wazi kwamba aliwahi kuwa na mpango wa kununua mtandao huo lakini baada ya Elon Musk kununu mtandao huo, hali ikawa tofauti kiasi cha kuhisi hatoweza tena kununua mtandao huo kwani nafasi ya yeye kununua mtandao huo kwa sasa ni ndogo ukilinganisha na kipindi unamilikiwa na Jack Dorsey.