Posh afunguka alikoipata shepu yake

Jumanne , 22nd Jan , 2019

Mlimbwende maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini, Posh Queen, ameweka wazi chanzo cha kuwa na shepu ya kuvutia, baada ya tuhuma nyingi kuibuka kuwa ametumia dawa za kichina kuipata.

Akizungumza na www.eatv.tv, Posh amesema kwamba hivyo ndivyo alivyozaliwa na sio madawa, na kuhusu picha zinazomuonesha akiwa hana hiyo shepu, alikuwa mwembamba sana kiasi cha kushindwa kuonekana jinsi alivyoumbika.

“Zile picha zinaonesha nilikuwa mwembamba, sasa mtu mwembaba anakuwaje na shepu!?. Watu wanataka iwaje!?, mwisho wa siku ni mwili wangu,  sijatumia mchina au kitu chochote, ni kazi unakaa kila siku unajustify, lakini mtu anavyotaka kufikiri ni uamuzi wake”, amesema Posh.

Hivi karibuni zimezagaa picha za msichana huyo za zamani akionekana hana shepu, kitendo kilichowashangaza wengi ukilinganisha na muonekano wake wa sasa.