Jumamosi , 20th Jan , 2024

Mwaka 2011 nchini Italia, mtu asiye na uwezo wa kifedha (fukara) alijikuta matatani baada ya kukabiliwa na kesi ya wizi wa soseji na jibini ambazo zote kwa pamoja zilikuwa na thamani ya (€ 4) ambayo ni sawa na TZS 10,940 na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita (6) jela,

 

Lakini baada ya kesi hiyo kusomwa kwa mara ya tatu mahakamani hapo, Mahakama iliridhia kutupilia mbali shitaka hilo. 

Mahakama kuu ya Cassation nchini Italia, walitupilia mbali kesi hiyo kwa kile wanacho amini ya kuwa kila binadamu anayo haki ya kuishi, na kwenye jamii ambayo imestaharabika ubinadamu ni lazima kiwe kipaombele na hakuna mtu ambaye anapaswa kukabiliwa na njaa.

Unahisi ni wazo zuri ambalo linafaa kuigwa?

Picha: quotesgram.com