Jumatatu , 13th Sep , 2021

Baada ya siku za hivi karibuni Papaa Mopao, Barnaba Classic kuingia kwenye trend na vazi la sketi ambalo ni maalum kwa ajili ya wanawake, sasa una ambiwa huko Fiji, Kusini mwa Pasifiki vazi hilo huangaliwa kama vazi la kitaifa.

Picha ya Pamoja Waziri Mkuu wa Fiji Frank Bainimarama (kushoto) na Rais wa China H.E Xi Jinping

Vazi Sulu Vakataga ni kwa ajili ya wanaume na liliingia katika Taifa hilo na wamishonari waliokuwa wakitoka Tonga huku wakati mwingine sketi hizo hukatwa katwa upande wa chini.

Ikumbukwe pia Waziri mkuu wa Fiji, Frank Bainimarama wakati alipohudhuria Mkutano wa Shirika la Umoja wa mataifa la makazi mjini Nairobi 2019 alitinga vazi hilo na kuwashangaza watu wengi.