Talaka yamtajirisha Melinda Gates

Alhamisi , 6th Mei , 2021

Aliyekuwa mke wa bilione Bill Gates, Melinda Gates kuwa bilionea mpya hii ni mara baada ya kuhamishiwa kiasi cha fedha $1.8 B, takribani trilioni 4.1 kwenye akaunti yake toka kwenye kampuni ya Bill Gates kama mnufaika wa hisa za uwekezaji.

Melinda na Bill Gates

TMZ wameonesha namna kiasi hicho cha fedha kimepatikana, huku kampuni ya magari ya bilionea Bill Gates (Cascade Investment) imeripotiwa kuhamisha kiasi hicho cha fedha siku ya jumatatu Mei 3, siku ambayo walitalakiana.

Baada ya kiasi hicho cha fedha kuhamishwa taarifa zinasema utajiri wa Bill Gates umeshuka hadi kufikia $130.4 B, lakini bado inamuweka tajiri huyo kwenye nafasi ya 4 katika orodha ya matajiri wa dunia.