"Ukitaka kuoa lazima uwe na kazi" -Charles Nduku

Jumanne , 5th Mei , 2020

Mtaalam wa masuala ya biashara Charles Nduku, amesema kuwa mwanaume yeyote ambaye anataka kuoa ni lazima awe na kazi ambayo itamuwezesha kumudu gharama za maisha na kuisimamia vyema familia yake.

Mtaalam wa Masuala ya Biashara, Charles Nduku

Hayo ameyabainisha wakati akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ cha EATV, kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa na kusema kuwa moja ya sababu inayofanya mwanaume ashindwe kumudu majukumu ya familia yake ni kutokufanya kazi hivyo ni vyema kutafuta kazi ambayo itaweza kumpa kipato.

"Hata Biblia inasema kwamba, ukitaka kuoa ni lazima uwe na kazi siyo uwe umeajiriwa ila ni wajibu wa wewe kutimiza majuku ya familia yako, kazi yoyote ambayo utakuwa unaifanya na kukuingizia kipato, ni lazima uzalishe na usipofanya hivyo lazima familia itakukimbia" amesema Charles Nduku.

Aidha Charles Nduku ameongeza kuwa wanaume huwa wanajisikia vizuri sana kuhudumia wanawake zao, hivyo mwanaume akiona mwanamke ndiyo anahudumia familia huwa anajisikia vibaya.