Wafahamu wapenzi mavampire wanaoishi hadi sasa

Jumatano , 13th Mar , 2019

Neno Vampire sio geni masikioni mwa wengi, hasa wale wafuatiliaji wa filamu mbali mbali hasa za kutisha.

Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali zilizofanywa na wataalamu wa masuala ya utafiti kutoka chuo kikuu cha Havard cha Marekani, Vampire ni viumbe ambao mpaka sasa inaaminika ni 'myth' (hadithi za kusadikika) ambao waliwahi kuwepo kwenye karne ya 17, huko barani Ulaya.

Viumbe hawa walisaidikika kuwa moja ya tishio kubwa sana kwa uhai wa watu, kutokana na kunyonya damu za watu na kuzinywa hadi mtu huyo anakufa, au na yeye kubadilika kuwa vampire.

Kama ambavyo bado inaaminiwa ni viumbe wa kusadikika kwa sababu hakukuwa na 'ushahidi mkubwa' wa uwepo wao, lakini hivi sasa dunia nzima ukitaja neno vampire lazima itajulikana ni kiumbe gani anazungumziwa.

Wapenzi vampire

Hili linawezekana likawa la ajabu lakini ukweli ni kuwa huko nchini Uingereza wapenzi wawili wameaminika kuwa na chembechembe za viumbe hawa hatari, kutokana na kuwa na tabia kama zao za kunywa damu za watu.

Ingawa mpaka sasa hakuna tukio la mauaji lililoripotiwa kuwahi kulifanya, lakini wapenzi hawa wanaojulikana kwa majina ya Lia Benninghoff (26) na Aro Draven (44) wamekuwa wakinywa damu zao kama chakula chao ambacho wenyewe wanadai ndio uhai wao.

Lia anasimulia kwamba alikutana na Aro kwenye mtandao wa kijamii na wakapanga kuonana, na alipomwambia kwamba yeye ni vampire akafurahia na kumuomba amgeuze ili wafanane.

“Kuanzia muda tulionana na tu, nilijua yeye ndiye, na aliponiambia kuwa yeye ni vampire nilishangazwa na kufurahi, sikuwahi kuamini kuwa vampire wapo, ingawa nilitumaini sana wapo”, alisema Lia.

“Aliponiambia kushea damu itatufanya tuwe karibu zaidi, nilimuomba anibadilishe, Aro akajikata na kiwembe nyuma ya mkono wake na kunipa damu, kisha nikajikata nami nikampa yangu akanywa, ghafla nikajisikia nguvu ya ajabu ndani yangu, ilinichukua siku nzima kubadilika, ilikuwa ni maajabu lakini ni nzuri zaidi kuliko ngono”, aliendelea kusimulia Lia.

Lia aliendelea kusimulia kuwa anapenda sana maisha hayo na kwa sasa anakunywa hadi mara nne kwa wiki, na asipokunywa hujihisi mdhaifu.

Hata hivyo wapenzi hao huwa wananunua nguruwe kwa ajili ya kupata damu ya kunywa, na pia huwa wanakunywa damu zao wenyewe tu, na sio za watu wengine.

Familia za wawili zimekubaliana na hali zao, baada ya vipingamizi vikubwa kutoka kwa wazazi wa Aro, ambao waliweka wazi kuwa walimuasili mtoto huyo alipokuwa na miaka mitano.

Lia na Aro wakinyonyana damu