Jumatano , 19th Oct , 2022

Vijana wawili wanaojiita za The Ramadhan Brothers, ambao video yao ilisambaa mitandaoni wakiwa kwenye mashindano ya Australia got talent, na kubonyezewa Golden Buzzer baada ya kufanya mazuri wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa namna ambavyo imekuwa ikiwatia moyo wasanii.

The Ramadhan Brothers wakiwa kwenye studio za East Africa Radio

Kauli hiyo wameitoa hii leo Oktoba 19, 2022, wakati wakizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio ambapo kwa pamoja wameeleza safari yao ilivyokuwa na jinsi ambavyo milango imefunguka na wamekuwa wakialikwa kwenye mashindano mbalimbali.

"Napenda sana kuwashukuru viongozi wote wa Tanzania akiwemo Rais Samia kwa kututia moyo sisi wasanii, kusema kweli serikali yetu inatia nguvu sana na ina-support sana wasanii, tuna-show moja kubwa sana, tuna nusu fainali na fainali yenyewe nina imani Watanzania watashangaa kuona tunafanya maajabu yale," wamesema The Ramadhan Brothers

Aidha wameongeza kuwa, "Hatua tuliyofika kusema kweli tunamshukuru Mungu ni hatua kubwa sana na kwa sasa hivi tulipofikia ile show ni utambulisho, na pale kulikuwa na wasanii zaidi ya 300 lakini The Ramadhan Brothers tumekuwa wasanii wa kwanza kutunukiwa tuzo ya golden buzzer,".