Jumanne , 18th Dec , 2018

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, mama Anna Mghwira amewataka wananchi wenye asili ya mkoa wa Kilimanjaro kwenda mkoani humo kwa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, kwani kuna kitu maalum amewaandalia.

Akizungumza na www.eatv.tv, mama Mgwira amesema kwamba wanakusudia kufanya tamasha kubwa ambalo litawakutanisha wakazi wa mkoa huo, ambalo litatumika kuhamasisha kutangaza vitu mbali mbali vilivyomo mkoani humo.

"Wajiandae tu waje, kutakuwa na tukio kubwa la kimkoa, kama tamasha hivi la kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya, kutakuwa na vitu mbalimbali, shughuli za kitamaduni, ngoma, vyakula na maombi kwaajili ya mkoa huo, pia tutakuwa na kikao kibwa cha wawekezaji na shamrashamra," amesema Mama Anna Mghwira.

Mama Mgwira ameendelea kusema kuwa mwaka jana waliandaa tamasha hilo na lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, lakini mwaka huu wameliandaa mapema, hivyo ni vyema wana Kilimanjaro kwenda kwa wingi kwaajili ya kukutana na kupanga mipango ya kimaendeleo.