Jumanne , 14th Mei , 2019

Wamiliki wa mtandao wa kijamii wa 'Whatsapp' wamegundua shambulio la kimtandao lililolenga kuiba taarifa za watumiaji wa mtandao huo kwa kutumia program zililzoanzishwa na wadukuzi hao, hivyo kuagiza watumiaji kuzipakua upya program zao.

Nembo ya Whatsapp

Imeripotiwa kuwa uvamizi huo wa mtandao wa WhatsApp ulibuniwa na kampuni ya usalama ya Israeli inayofahamika kama NSO Group, kampuni ambayo awali ilielezewa kama 'Cyber arms dealer'.

Shambulio hilo dhidi ya WhatsApp, limegunduliwa mapema mwezi huu, lilikuwa ni la kwanza kuwahi kuripotiwa katika gazeti la Financial Times. Ambapo wadukuzi wanaweza kuweka programu ya kuchunguza taarifa kwenye simu yako na vifaa vingine vinavyotumiwa kwa kutuma ujumbe wa WhatsApp.

Mtandao huo umewaomba watumiaji wake ambao ni zaidi ya watu bilioni 1.5 kufungua upya App zao kama njia sahihi ya kuepuka udukuzi huo, na WhatsApp imesema ni mapema kujua ni watumiaji wangapi wameathiriwa na udukuzi huo.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Kampuni ya Facebook Inc ambayo inamiliki mtandao huo, WhatsApp ina jumla ya watumiaji bilioni 1.5 kote duniani.