Ijumaa , 19th Oct , 2018

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya tayari imeshabainika kuwa ugonjwa wa Saratani ya matiti hauishii tu kwa kina mama bali huwapata hata wanaume huku pia ikitajwa kuwa Saratani ya kurithi ni hatari kwenye ukoo.

Picha ya matibabu imetumika kama mfano na haihusiani na Saratani.

Akiongea leo kwenye MJADALA wa East Africa Television, Dr. Deogratius Mwanakulya ambaye ni daktari bingwa wa Saratani kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili, amezitaja dalili za Saratani ya matiti ambayo ni ya kurithi kwenye familia.

''Aina hii ya Saratani inatokea kwa mtu kurithi vinasaba kutoka mtu mmoja hadi mwingine ambapo kizazi cha kwanza kinabeba taarifa na kupeleka kizazi kinachofuata'', - amesema.

Aidha Dr. Mwanakulya ameongeza kuwa mtu anaweza kutambua kama familia yake ipo kwenye kundi hili kwa kupitia kuangalia idadi ya ndugu ambao wana tatizo hilo kwenye familia au ukoo ama unaweza kujua kwa kupitia mwanaume kwenye kupata Saratani ya matiti jambo ambalo ni nadra sana.

Dalili nyingine iliyotajwa ya kujua kama aina hii ya Saratani ipo ndani ya familia yako, ni mtu mwenye umri mdogo kupata Saratani jambo ambalo sio la kawaida kwani Saratani mara nyingi huwapata watu wenye umri mkubwa zaidi.

Zaidi mtazame daktari hapo chini akifafanua zaidi.