Nyota wa zamani wa Argentina Sergio Aguero
Aguero mwenye umri wa miaka 33, ameichezea Argentina michezo 101 na kufunga magoli 41 huku akiitumikia kwenye michuano mitatu ya kombe la dunia (2010,2014 na 2018) sambamba na kutwaa kombe la Copa America mwaka 2021 alitangaza kustaafu soka kutokana na matatizo ya moyo akiwa na klabu yake ya Fc Barcelona
"yalikuwa mazungumzo mazuri na Chiqui (Rais wa AFA),bado hatujajua nitakuwa kwenye nafasi gani lakini nitakuwepo na timu kwenye michezo ya kombe la dunia.Napenda kutumia muda mwingi na wachezaji maana nimetoka nao mbali sana na natamani kuwa karibu nao na kujaribu kutoa mchango wangu ili timu ya taifa ifanye vizuri zaidi" amesema Aguero.
Argentina tayari washafuzu kushiriki kombe la dunia nchini Qatar wakiwa hawajapoteza mchezo wowote wakifuzu na Brazil kupitia kanda ya America kusini huku hatma ya Sergio Aguero kuwemo kwenye benchi la ufundi la Argentina itajulikana wiki mbili zijazo.





