Alaba akubali kujiunga na Real Madrid

Jumatano , 21st Apr , 2021

Mlinzi wa Bayern Munich, David Alaba amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Real Madrid ifikapo wakati wa majira ya kiangazi msimu huu.

Mlinzi wa Bayern Munich, David Alaba akiwa kwenye majukumu ya kuitumikia klabu yake.

Alaba atasaini mkataba wa miaka mitano na Los Blancos ambao utamuweka nchini Hispania hadi majira ya joto ya mwaka 2026.

Taarifa hii inamalizia sakata la muda mrefu juu ya hatma ya nyota huyo ambaye mapema mwaka huu alithibitisha kuwa angeondoka nchini Ujerumani lakini haikufahamika angejiunga na klabu ipi.

Nyota huyo raia w Australia ambaye ameitumikia The Bavarians kwa takribani miaka 13 kwa mafanikio, alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu sasa na kuhamia nchini Hispania huku Barcelona nayo ilikuwa ikiwania saini yake.