Alichokisema Kaseja juu ya usajili wa Ajibu?

Jumatano , 5th Aug , 2020

Nahodha na mlinda mlango wa klabu ya KMC ,Juma Kaseja amesema milango ipo wazi kwa nyota wa klabu ya Simba, Ibrahim Ajibu kujiunga na klabu hiyo yenye maskani yake Kinondoni Jijini Dar es salaam iwapo benchi la ufundi litapendekeza usajili wake.

Ibrahim Ajibu (Kushoto) akinyanyua kombe la VPL pamoja na Nahoha wake John Bocco (Kulia) .

Kaseja ambaye alicheza kwa nyakati tofauti kwenye vilabu vya Simba na Yanga kwa mafanikio ameiambia Kipenga kuwa KMC ni Timu ya Wananchi hivyo milango ipo wazi kwa mchezaji yeyote atakayehitajika .

Mlinda mlango huyo mzoefu ambaye pia yupo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, amesema Ajibu ni mchezaji mwenye kiwango kizuri na anahitaji kupata nafasi ila na yeye aongeze jitihada na anaweza kucheza katika timu yoyote.

Ajibu ambaye hajawa na wakati mzuri katika kikosi cha Simba anahusishwa kuhitajika katika vilabu vya KMC na Azam zote zilizopo ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara.

Katika hatua nyingine Kaseja amewataka wachezaji kufanya maamuzi sahihi katika kipindi hiki cha usajili ambapo vilabu vinasaka saini za wachezaji ili kujiimarisha kabla ya kuanza kwa msimu mpya.