
Samatta na Alikiba
Mchezo huo utapigwa mnamo Juni 2, 2019 ambapo Alikiba na wachezaji aliowachagua wanaomuunga mkono watacheza na timu ya Samatta ikiwa ni katika taasisi yao ya 'Samakiba Foundation' yenye lengo la kusaidia jamii yenye mahitaji, ikiwemo watu wenye ulemavu na watoto yatima.
Mbwana Samatta amesema, "lengo letu sisi ni kusaidia jamii na tunawaomba watanzania wajitokeze kusaidia na pia tusaidiane kupeleka taarifa watu wajtokeze lakini nafikiri inajulikana anayefungwa ni nani, kwahiyo hata mkienda kusema huko mnaweza kuweka matokeo yoyote yale, game itakuwa Jumapili lakini mtu atafungwa nne".
Naye kwa upande wake Alikiba amemjibu Samatta kwa kumtambulisha kocha wa kikosi chake raia wa kigeni, akiahidi kuwa kutokana na kikosi chake lazima wataifunga timu ya Samatta.
"Mechi yetu ya mwaka uliopita walitufunga kwa mbinde tuu. Ilibidi tu niwaambie wachezaji wangu waachie kidogo sababu tulikuwa tunacheza na Championi kwahiyo tulitaka tusimdhalilishe", ameongeza Alikiba.
Pia Samatta na Alikiba wamesema watakaa na kupanga vizuri namna ya kusaidia timu ya taifa ya watu wenye ulemavu ambayo inatarajia kushiriki michuano ya Kimataifa hivi karibuni. Pia watu wenye ulemavu wataingia bure katika mchezo huo.