Ijumaa , 27th Aug , 2021

kocha wa Juventus Massimiliano Allegri amethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo anatakakuondoka klabu hapo, na tayari ameshawaaga wachezaji wenzake na mchezaji huyo bora mara tano Duniani anaripotiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na mabingwa wa England Manchester City.

Cristiano Ronaldo

Allegri alithibitisha nia ya Ronaldo kutaka kuondoka Juventus kwa kusema ‘’Jana, Ronaldo aliniambia kuwa hana nia tena ya kuichezea Juventus, na hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho dhidi ya Empoli. Atatafuta klabu nyingine baada ya miaka mitatu hapa.'’

Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, alitumia dakika 40 kuwaaga wachezaji wenzake laeo asubuhi kabla ya timu hiyo kuaanza ratiba ya mazoezi na inaripotiwa amechukua vitu vyake vyeto, na ameshafikia makubaliano na klabu ya Manchester City na atasaini mkataba wa miaka miwili (2).

Usajili wa Ronaldo kujiunga na Manchester City umefuatia baada ya mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ambae ndio alikuwa chuguo la kwanza la mabingwa hao wa England kwenye usajili wao wa nafasi ya mshambuliaji, kuthibitisha kuwa hataondoka katika klabu hiyo na yupo tayari kuisaidia Spurs kwa asilimia 100 kufikia malengo yake msimu huu.

Kuondoka kwa Ronaldo Juventus ni pigo kwa mashabiki lakini itakuwa ni hauweni kwa klabu hiyo kupunguza bajeti ya mishahara ya wachezaji, na ada ya uhamisho ya mchezaji huyo inatajwa kuwa ni pauni milioni 25.