
Xabi Alonso anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa Borussia Monchengladbach
Alonso ambaye ni kiungo mchezeshaji wa zamani wa Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich wamekubaliana vipengele vyote muhimu ili kujiunga na timu hiyo ya Monchengladbach kilichobaki ni kutangwaza tu.
Kwenye eneo la ukocha Alonso hajakuwa na uzoefu mkubwa katika nafasi hiyo, kwa sasa alikuwa kocha wa kikosi cha pili cha klabu ya soka ya Real Sociedad anakwenda kuiongoza timu ya ligi 'bundesliga' yenye ushindani mkubwa
Alonso kiungo fundi aliyewavutia mashabiki wengi duniani akiwa mchezaji, huwenda akapoteza heshima yake kwenye eneo hili la ukocha kama hata pata mafanikio, wadadisi wa mambo wanaona klabu ya Monchengladbach walipaswa kuajiri kocha mwenye uzoefu ili angalau waweze kufuzu mashindano ya Ulaya
Pamoja na Xavi kujiunga ana timu hii mahususi kwa msimu ujao, kwa sasa Moenchengladbach ipo kwenye nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi wenye timu 18 huku ikiwa na alama 36 katika michezo 26