Amad Dallo na Michael Carrick
Kiungo huyo wa zamani alichukua jukumu la kocha mkuu baada ya kuondolewa kwa Ruben Amorim na amefanikisha matokeo mazuri ushindi mara nne na sare moja katika michezo mitano na kupeleka Man United kwenye nafasi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Amad alisema Carrick ni muhimu kwa sababu anajua klabu vyema, anawasihi wachezaji kucheza kwa ajili yao na mashabiki.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa Jonny Evans kurudi kama sehemu ya benchi la ufundi, akibainisha kuwa uzoefu na uelewa wake wa klabu ni wa thamani kwa wachezaji.
Man United wanatarajia kuendeleza mwendelezo mzuri Jumatatu ijayo watakapokutana na Everton FC.





