Alhamisi , 24th Jun , 2021

Pitia taarifa za michezo mbalimbali zitokanazo na namba ambazo pia unaweza kuzisikiliza kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa moja na robo asubuhi kupitia kipindi cha Super Breakfast cha East Africa Radio.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo akishangilia bao .

6 – Ni idadi ya medali za dhahabu anazomiliki mwana mama Allyson Felix baada ya kuwa bingwa wa riadha mara 6 kwenye michuano ya Olympic, ameibuka na kusema kwa sasa ameachana na kampuni ya NIKE iliyokuwa ikidhamini viatu vyake na sasa amesema atakuja na viatu vipya vyenye udhamini wake yeye binafsi.

5 – Ni idadi ya makocha ambao wamembwaga chini na Lucien Farve na kocha huyo raia wa Uswizi anatarajiwa kutangazwa rasmi baada ya masaa chache kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na kopcha Roy Hodgson ambaye alihudumu klabuni hapo kwa muda wa miaka mitatu tokea mwaka 2017 hadi alitangaza kuondoka klabu hapo mwishoni mwa msimuu mwaka 2020-2021.

4 – Hii ni mara ya nne klabu ya Tottenham Hotspurs kufanya mazungumzo na kushindwa kuafikiana na makocha wanne kwani usiku wa kuamkia leo wameshindwa kukubaliana na aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Hispania na sasa Sevilla, Julen Lopetegui baada ya wiki zilizopita kushindwa kukubaliana na Antonio Conte, Genarro Gattuso na Paul Fonseca.

3 – Ni utofaui wa alama kati ya timu ya Atlanta Hawks iliyoibuka na ushindi wa alama 116-113 ikiwa ugenini mbele ya Milwaukee Bucks kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa fainali ya ukanda wa Mashariki kwenye ligi ya kikapu nchini Marekani maarufu 'NBA' huku bwana mdogo, Trae Young akiibuka nyota wa mchezo kaw kufikisha alama 48, rebaundi 7 na assisti 11.

2 – Ni idada ya mabao waliyoyapata timu ya taifa ya Brazil mbele ya timu ya taifa ya Colombia kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya COPA Amerika na mabao hayo kufungwa na Roberto Firmino na Casemiro huku lile la kufutia machozi la Colombia limefungwa na Luis Dias. Kwa matokeao hayo Brazil imefikisha alama 9 na kuwa kinara wa kundi B.

Mchezo mwengine wa michuano hiyo ni ule uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 kati ya Ecuardo na Peru.

1 – Ni idadi ya bao ambalo nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo anasaka kulifunga ili mfungaji bora wa muda wote kwa upande wa timu za taifa baada ya usiku wa jana kufunga mabao 2 kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Ufaransa kwenye michuano ya Ulaya na kuifikia rekodi ya mshambuliaji wa Iran, Alli Deai mwenye mabao 109 sawa na CR7 kwasasa.

CR7 anafursa ya kuipiku rekodi hiyo kwasababu timu yake ya Ureno imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambapo imepangiwa kucheza dhidi ya Ubelijigi June 27, 2021.