Ijumaa , 4th Dec , 2020

Klabu ya Arsenal ya Uingereza imeweka rekodi ya kushinda michezo mitano ya hatua ya makundi na kufikisha alama 15 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanya hivyo tokea mwaka 2005-06 ambapo walifanikiwa kufika fainali ya michuanoo ya klabu bingwa ulaya na kupoteza 2-1 kwa FB Barcelona.

Nyota wa Arsenal, wakiongozwa na nahodha Pierre- Emerick Aubameyang wakishangilia ushindi.

Arsenal wameweka rekodi hiyo baada ya kuifunga klabu ya Rapid Vien mabao 4-0 usiku wa kuamkia hii leo kwenye mchezo wa mzunguko wa tano wa michuano ya Europa league. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Alexander Lacazette, Villar, Nketian na Smith-rowe.

The Gunners imefuzu kucheza hatua inayofuata ya mtoano ya 32 bora kabla ya mchezo wa usiku wa hapo jana lakini licha ya kiwango kizuri wanachokionesha kwenye michuano hiyo baadhi wa mashabiki wa klabu hiyo wamesema wanamtaka Mesut Ozil arejeshwe kikosini.

Mashabiki hao hawakubaliani na uamuzi wa kocha Mikel Arteta kumtema kikosini kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao kwa kudai hayupo kwenye mipango yake jambo ambalo linawafanya washika mitutu hao wa jiji la London kutofunga mabao mengi.

Katika mchezo huo mashabiki takribani elfu mbili waliruhusiwa kuingia katika uwanja wa Emirate kuishuhudia mchezo huo.

Vilabu vingine 17 vilivyocheza usiku wa hapo jana na kujihakikishia kufuzu hatua ya mtoano ya 32 bora ni pamoja na AS Roma, Slavia Prague, Bayer Leverkusen, Rangers, Benifica, Granada, PSV Eindhoven, SSC Napoli, Leicester City, SC Braga, Lille, AC Milan, Villareal, Royal Antwerp, Dinamo Zagreb, Hoffenheim na FK Crvena Zvezda.

Vilabu vingine 14 vinalazimika kusubiri kujua hatma yao ya aidha kufuzu ama kutofuzu baada ya kucheza michezo ya mwisho ya kukamilisha hatua ya makunndi inatayotaraji kuchezwa katikati mwa mwezi Huu.