Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Arsenal yaendeleza unyonge, yachapwa nyumbani

Jumapili , 12th Aug , 2018

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka ya England, Manchester City, wameanza mbio za kutetea ubingwa wao kwa kushinda ugenini dhidi ya Arsenal kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliomalizika usiku huu.

Wachezaji wa Arsenal baada ya mchezo dhidi ya Man City.

Manchester City ambayo iliwaanzisha benchi nyota wake kadhaa waliokuwa katika kikosi cha kwanza msimu uliopita kama Kevin De Bruyne, Gabriel Jesus, Nicolás Otamendi na Leroy Sané ilitangulia kwa bao la Raheem Sterling dakika ya 14, kabla ya Bernardo Silva kuongeza la pili dakika ya 64.

Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery amepoteza mechi yake ya kwanza ya ligi kwenye uwanja wa nyumbani hivyo kuanza vibaya kibarua chake ambacho amekichukua kutoka kwa Arsene Wenger ambaye alikuwa na uzoefu wa ligi kuu ya EPL kwa zaidi ya miaka 20. Katika mechi 6 za hivi karibuni Arsenal imepoteza 4 na sare 2 dhidi ya Man City.

Bao la Bernardo Silva leo, limemfanya nyota huyo kufikisha mabao matano katika mechi zake  za mwisho alizoanza. Hii imekuja baada ya nyota huyo wa Ureno kushindwa kufunga bao hata moja kwenye mechi zake 9 za kwanza ndani ya kikosi hicho.

Wachezaji John Stones (Man City) na Mesut Ozil (Arsenal) wakiwa kumiliki mpira.

Muingereza Raheem Sterling yeye amefunga bao lake la 50 kwenye ligi kuu ya Englanda huku likiwa bao lake la 3 kufunga nje ya boksi. Man City sasa imeungana na timu zingine kubwa ambazo zimepata ushindi kwenye mechi zake za ufunguzi ambazo ni Manchester United, Chelsea, Liverpool na Tottenham.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali