
Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Michael Zorc amesema Aubameyang ameachwa kwa sababu hana utayari na mchezo, kutokana na mambo mengi kuhusu usajili yanayomkabili hivyo si vizuri kumjumuisha kenye timu.
''Hauwezi kwenda Berlin na Pierre, ana mambo mengi yanamkabili kuhusu usajili na hana utayari wa mchezo hivyo hatudhani kama ataisadia timu kwenye mchezo dhidi ya Hertha Berlin'' amesema Zorc.
Hatua hiyo ya Dortmund kumuacha Aubameyang inachukuliwa kama ni sehemu ya nyota huyo kushughulikia uhamisho wake kuelekea klabu ya Arsenal.
Kwa upande mwingine Mkurungenzi huyo amemtaka kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuacha kuongelea wachezaji wa timu nyingine bali afanye majukumu yake ya kufundisha Arsenal. Hatua hiyo imekuja baada ya jana Wenger kusema Aubameyang anaweza kufanya vizuri akijiunga na Arsenal.