Baada ya jana usiku klabu ya Azam FC kumaliza mazoezi yake tayari kwa mchezo huo, mlinzi huyo akakweka wazi kuwa wanachohitaji wao ni ushindi tu kwani mechi hiyo ya hatua ya 16 inahitaji mshindi tu ndio asonge mbele hivyo lazima washinde.
Maneno hayo ya Bruce Kangwa yamekuja ikiwa Azam FC haijashinda mechi hata moja kati ya tatu zilizopita ambazo zote zilikuwa za Ligi Kuu, ikitoka sare mbili dhidi ya Kagera Sugar 1-1 na Lipuli 0-0, pamoja na kufungwa 1-0 na Simba SC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi. Azam FC ndio timu iliyocheza fainali ya kwanza ya michuano hiyo msimu wa 2015/16 lakini ikafungwa na Yanga ambao waliibuka mabingwa.
KMC ni timu iliyopo chini ya Manispaa ya Kinondoni na imepanda kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi kuu kuanzia msimu ujao ikiwa chini ya kocha mzoefu Felix Minziro.



